Sports and Entertainment

Jumanne, 28 Oktoba 2014

Mkutano wa Halima Mdee waingia dosari

Hakuna maoni :
Mkutano wa mwenyekiti wa baraza la wanawake  wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee umeingia dosari baada ya vijana wanaodaiwa kuwa niwafuasi wa chama cha mapinduzi CCM kuingia na mabango yao katika mkutano uliokuwa ukifanyika kijiji cha Kyamiorwa kata Kashalunga  wilayani Muleba na kusababisha vurugu.
Mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema Halima Mdee amepokelewa leo katika kijiji cha Kyamiyorwa na kufanya mkutano na wananchi katika kijiji hicho ambapo vijana wanne wanaodaiwa kuwa nifuasi wa chama cha mapinduzi CCM walipoingia katika mkutano huo huku wakiwa wameshikilia mabango yao na kusababisha vurugu katika mkutano huo, vurugu hiyo zimetulizwa na jeshi la Polisi na mpaka sasa jeshi la Polisi lina mshikilia kijana mmoja aliyetambulika kwajina la Mansud Amri ambae ametajwa kuhusika katika kufanya vurugu hizo.
 
Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti wa bara la wanawake wachama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Halima Mdee amewataka vijana kutotumiwa na wanasia wanao lenga kuvuruga amani ya nchi na badalayake watulie ili kujenga taifa lenye amani na utulivu.
 
Nao baadhi ya wafuasi wa chama hicho akiwemo mbunge wa viti maalumu Conchester Rwamlaza wamewataka wananchi kutoiunga mkono katiba mpya na akaongeza kuwa wananchi wanatakiwa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuhakikisha wana chagua viongozi bora ambao wataliongoza taifa hili kwa umakini.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni