Jumanne, 28 Oktoba 2014
Nahodha Bafana bafana apigwa risasi na maharamia na kupoteza uhai

Mpenzi wa Senzo Meyiwa, mwanamuziki Kelly Khumalo, siku ya Jumapili alituma picha akiwa pamoja naye kabla hajauawa.
Nahodha wa timu ya Afrika Kusini na mlinda mlango Senzo Meyiwa amefariki baada ya kupigwa risasi, wamesema polisi wa Afrika Kusini.
Tukio hilo liliripotiwa kutokea kwenye nyumba ya mpenzi wa Meyiwa, Vosloorus, kusini mwa Johannesburg.

Kelly Khumalo akiwa amembeba mtoto akiwasili nyumbani kwake katika mji wa Vosloorus kufuatia kifo cha Meyiwa.
Mlinda mlango huyo, 27, alikuwa akiichezea Orlando Pirates na alikwishaichezea Afrika Kusini katika mashindano manne ya kufudhu ya Kombe la Dunia.
Siku ya Jumamosi, alikuwa katika klabu, ambapo walifanikiwa kuvuka nusu fainali katika Kombe la Ligi ya Afrika Kusini.
Orlando Pirates waliifunga Ajax Cape Town 4-1.

Mlinda mlango Meyiwa aliichezea timu yake siku ya Jumamosi jioni kabla ya kupigwa risasi. Ameshawahi kuwa nahodha wa Afrika Kusini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni