Jumanne, 28 Oktoba 2014
Raisi wa kwanza mwanamke Brazil ashinda kwa awamu ya pili
Dilma Rousseff amechaguliwa tena kuwa rais wa Brazil, baada ya kupata kura zaidi ya asilimia 51 katika kinyang’anyiro kikali cha uchaguzi kwa miaka ya karibuni.
Uhesabuji rasmi ulimuonyesha mpinzani wake, mgombea wenye siasa za mrengo wa kati Aecio Neves, akipata asilimia 48 ya kura.
Katika hotuba yake ya ushindi, Bi Rousseff alisema alitaka kuwa “rais bora zaidi kuliko alivyokuwa mpaka sasa”.
Alipambana na maandamano mwaka uliopita dhidi ya rushwa, rekodi ya matumizi ya Kombe la Dunia na huduma duni.
Bi Rousseff, ambaye amekuwa madarakani tangu 2010, ni maarufu kwa Wabrazili maskini wanaomshukuru kwa huduma za ustawi kutoka serikalini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni