Sports and Entertainment

Jumapili, 30 Novemba 2014

Kutana na bilionea wa kichina aliyelipa fadhila kwa wanakijiji kwa kufanya kufuru hii...

Hakuna maoni :
 Xiong Shuihua
Bilionea  Xiong Shuihua akiwa ofisini kwake
Kutoa ni moyo na wala sio utajiri. Bilionea mmoja Raia wa China ameamua kuboreshea makazi ya watu waishio katika kijiji alichozaliwa  baada ya kubomoa nyumba zao walizokuwa wakiishi awali na kisha kuwajengea maghorofa ya kisasa ikiwemo na kuwapatia mahitaji ya msingi kama vile chakula kwa baadhi ya wasiojiweza.
Bwana Xiong Shuihua alizaliwa katika kijiji cha  Xiongkeng kilichopo kwenye mji wa Xinyu kusini mwa China na kusema kwamba familia yake mara zote imekuwa vizuri baada na kuungwa mkono na wakazi wa hapo katika kipindi chake cha utotoni.
Inaelezwa kuwa baada ya Bwana Shuihua kutengeneza mamilioni ya fedha kupitia sekta ya vyuma aliamua kujitolea kuisaidia jamii yake ambapo zaidi ya familia 72 zimeweza kupata makazi ya uhakika na kudumu.

Village Rebuilt To Give Mansions To Residents By Millionaire
Pichani ni maghorofa yaliyojengwa na bwana Shuihua  na wakazi waishio eneo hilo

Village Rebuilt To Give Mansions To Residents By Millionaire
Ghorofa za kifahari walizokabidhiwa familia zaidi ya 72 kutoka kwa bilionea Shuihua
Village Rebuilt To Give Mansions To Residents By Millionaire
Wanakijiji wa Xiongkeng wakipata msosi huku wakiwa kwenye mijengo yao ya maana
Village Rebuilt To Give Mansions To Residents By Millionaire
Moja ya eneo la kijiji cha Xiongkeng
Village Rebuilt To Give Mansions To Residents By Millionaire
Lango kuu la kuingilia kijiji cha Xiongkeng
Village Rebuilt To Give Mansions To Residents By Millionaire
Maisha bora kwa kila mchina

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni