Sports and Entertainment

Jumapili, 30 Novemba 2014

TETESI ZA USAJILI MAJUU

Hakuna maoni :

Mchezaji Yohan Cabaye yuko mbioni kurudi kwenye Ligi Kuu ya England.
Mchezaji Yohan Cabaye yuko mbioni kurudi kwenye Ligi Kuu ya England.
Kipindi cha baridi kinapokaribia kufungwa tetesi za usajili zimeanza kusikika kuanzia kwa wachezaji Yohan Cabaye, Edson Cavan pamoja na Lionel Messi.
Arsene Wenger anasema hajaingia sokoni kutafuta wachezaji wapya
Kocha wa Arsenal amesisitiza hawezi kukimbilia kuleta wachezaji wapya kwenye klabu kwenye kipindi majira ya joto licha ya wachezaji wake muhimu kuwa majeruhi.
Sunderland wanadhamilia kumchukua Schone kutoka Ajax
Kulingana na habari zinavyosema kiungo wa kati wa Ajax Lasse Schone yuko mbioni kuhamia kwenye klabu ya Sunderland.
Arsenal wana mnyatia kwa ukaribu Yohan Cabaye
Arsenal, Manchester United pamoja na Liverpool wapo kwenye harakati za kutaka kumsajili kiungo wa timu ya Paris saint-German Yohan Cabaye.
Valdes ataacha kufanya mazoezi na timu ya Manchester United
Mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Barcelona Victor Valdes amesema ataacha mazoezi kwenye klabu ya Manchester United.
Mourinho apinga uvumi wa Messi kuhamia kwenye Klabu yake ya Chelsea
kocha wa Chelsea jose mourinho amefunga mjadala wa habari za kwamba Messi atahamia Stamford Bridge msimu huu.
Arsene Wenger apinga uvumi wa Cech kuhamia Arsenal
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amepinga habari za kwamba timu yake imezamiria kumsajili mlinda mlango wa Chelsea kwenye kipindi cha majira ya joto.
Arsene Wenger amesema hakuna ofa yoyote iliyowasilishwa juu ya mchezaji wake Podolski
Kocha Arsenal amesisitiza kuwa ajapokea ofa yoyote inayohusu kuhitajika kwa mchezaji wake Lukas Podolski kwenda kwenye timu nyingine
Manchester United inamhitaji Endson Cavani
United haina mpango wa kumpatia mkataba wa muda mrefu Radamel Falcao kwenye majira ya joto,lakini wamezamilia kutoa kitita kikubwa kumsajili mshambuliaji wa timu ya Paris Saint-Germain Endson CavanI.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni