Sports and Entertainment

Alhamisi, 27 Novemba 2014

mpambano wa Mayweather na Pacquiao wazidi kunukia

Hakuna maoni :
Floyd Vs MannyBondia nyota wa Marekani mwenye rekodi ya kutokupigwa hata pambano moja, Floyd Mayweather Jr. ameanza kuonyesha hofu juu ya pambano lake dhidi ya mhasimu wake mkubwa bondia mfilipino ‘Manny Pacquiao’ litakalochezwa hapo mwakani.
Katika ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na mtandao wa Daily Mail ilimnukuu mkufunzi wa Pacquiao, Freddie Roach akisema amekubaliana na ombi la Mayweather la  kuwepo kwa kifungu cha pambano la marudiano ikiwa ni katika moja ya sharti  alilotaka lizingatiwe.
”Ufahamu wangu ni kwamba Floyd anasisitiza juu ya pambano la marudiano endapo akipigwa na  Pacquiao, ambapo naamini atapigwa. hiyo iko sawa kwetu”,  alisema Roach.
Hii sio mara ya kwanza kwa Mayweather kusisitiza  pambano la marudiano katika mikataba yake.  Itakumbukwa Mwaka 2013, bingwa huyo wa Dunia alifanya kama kile alichofanya sasa kwa bondia Robert Guerrero katika mpambano uliopigwa kwenye ukumbi wa MGM Grand Arena ingawa alifanikiwa kushinda.



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni