Jumamosi, 6 Desemba 2014
Ronaldo atwaa Tuzo nyingine

Cristiano Ronaldo aliweka picha hiyo Instagram akiwa na tuzo yake ya mfungaji bora wa mwaka 2013.
Cristiano Ronaldo anaendelea kupata heshima kutokana na mtindo wake wa kufunga magoli mengi.
Tuzo yake ya hivi karibuni imetoka kwenye Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Soka baada ya kufunga magoli 69 katika mashindano yote ya Real Madrid na Ureno na kuwa mfungaji bora wa mwaka 2013.

Ronaldo akifunga mkwaju wa penati kwenye mechi ya El Clasico dhidi ya Barcelona mwezi Oktoba Santiago Bernabeu.
Nyota huyo, 29 alipokea tuzo yake siku ya Alhamisi, na kuamua kuwaonyesha wafuasi wake wa Instagram.
Ronaldo alituma picha hiyo ikiwa na maneno “Najihisi heshima kushinda tuzo ya Mfungaji bora wa Dunia 2013 kutoka Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Soka. Asanteni wote”.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni