Jumamosi, 6 Desemba 2014
Aslay : Nyimbo zitadumu

Kundi la Bendi la Yamoto
MUONGOZAJI wa kundi la ‘Yamoto Band’ Asilahi Isihaka ‘Dogo Aslay,’ amesema wanakusudia kufanya maonyesho mengi na kutunga nyimbo zitakazodumu kwa muda mrefu.
Amesema haoni sababu, kundi lao lifanye muziki usiokubalika sokoni.
Akizungumza kutoka jijini Dar es Salaam, Aslay alisema siku zote wamekuwa wakijitahidi kutunga nyimbo ambazo zitadumu na zisizochuja.
“Sisi tunaangalia kitu gani jamii inapenda, ndio maana tunatunga nyimbo nyingi, hatuwezi kutunga wimbo mmoja na tuna nyimbo nyingi.
“Tunakuwa tunatoa kwa awamu, kuzidi kuwafanya mashabiki wajue bado kuna kazi nzuri zaidi,” alisema.
Alisema kama kuna msanii anahitaji kumshirikisha kwenye nyimbo zake milango ya makubaliano iko wazi kabla ya kuhafiki muafaka.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni