Jumamosi, 6 Desemba 2014
Sijali maneno ya wasionitakia mema

Malkia wa miondoko ya taarabu Isha Ramadhani akiwa na wasanii wenzake Barnaba pamoja na Khadija Kopa
MALKIA wa miondoko ya taarabu Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi,’ amesema hajali maneno ya watu wenye nia ya kumporomosha kimuziki.
Amesema kuwa anajiamini yeye ni msanii mzuri, mwenye mbinu za kumshawishi kila shabiki aweze, kupenda tungo zake.
Akizungumza kutoka jijini Dar es Salaam, Isha alisema anafahamu ana wapinzani wengi wenye mawazo ya kumporomosha kimuziki na kumuombea mabaya.
Lakini hawataweza na wataendelea kusubiri sana maana mambo yanazidi kumnyookea.
Malkia huyo wa taarabu aliendelea kusema ninajua nina wapinzani ambao hawakosi la kusema na mimi ninajiamini na mambo yangu yanazidi kunyooka, na nina imani bendi yangu itaendelea kusonga mbele.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni