Sports and Entertainment

Alhamisi, 26 Juni 2014

Muntari na Boateng wafukuzwa kambini Ghana kwa utovu wa nidhamu

Hakuna maoni :

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng wametimuliwa kwa utovu wa nidhamu.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng wametimuliwa kwa utovu wa nidhamu.
Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng wamefukuzwa kwenye kikosi cha Ghana kinachoshiriki Kombe la Dunia kwa utovu wa nidhamu.
Taarifa ya Chama cha soka cha Ghana ilieleza kuwa wachezaji wote “wamefukuzwa kwa muda usiojulikana”.
Boateng anayeichezea Schalke 04, amefukuzwa kwa kutoa viashiria vya matusi vilivyomlenga kocha Kwesi Appiah kipindi timu hiyo ikifanya mazoezi mjini Maceio”.
Naye Muntari ameadhibiwa kwa kosa linalodaiwa na FA kuwa “alimvamia mwanachama wa kamati kuu.”
Chama cha FA cha Ghana kiliongeza kwenye taarifa yake kuwa tukio la Muntari lilifanyika siku ya Jumanne kwa mwanachama wa utawala wa timu anayejulikana kama Moses Arma, ambaye alidai kushambuliwa na kiungo huyo, 29.
Na Boateng, 27, kiungo na mzaliwa wa Ujerumani, chama cha FA kimesema “hajaonyesha kujutia vitendo vyake”.
Taarifa hizo zimekuja baada ya serikali ya Ghana kutuma kiasi cha fedha taslimu dola milioni 3 kwa ndege hadi Brazil ili kuliwalipa wachezaji fedha zao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni