Jumanne, 15 Julai 2014
Blatter amuhurumia Suarez
Sepp Blatter ana matumaini ya kumuona Luis Suarez akirejea uwanjani hivi karibuni.
Suarez alitolewa mapema kwenye Kombe la Dunia kwa aibu baada ya kumng’ata Giorgio Chiellini kwenye hatua ya makundi kati ya Italia na Uruguay.
Hiyo ilikuwa mara ya tatu kumng’ata mchezaji, kamati ya nidhamu ya FIFA ilimfungia mshambuliaji huyo wa Barcelona kujihusisha na shughuli zote za soka kwa miezi minne.
Kumekuwa na kilio nchini Uruguay kutokana na adhabu hiyo, ila Blatter alisema rekodi ya adhabu hiyo ilifanyika nje ya mikono yake.
Rais huyo wa FIFA alimpa pole Suarez kwa kukosa mashindano ya mwanzoni, na ana matumaini mshambuliaji huyo wa Uruguay atakuwa tayari na kudhamiria kulitumikia taifa lake hivi karibuni.
“Kama mchezaji, adhabu yake inanihusu mimi pia… inaumiza, inaumiza”, alisema Blatter kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mjini Rio.
“Ila kama rais wa FIFA sina budi kukubaliana na maamuzi yaliyochukuliwa na kamati huru”.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni