Sports and Entertainment

Alhamisi, 24 Julai 2014

Kaseja,Barthez,Dida watauana kugombea namba Yanga

Hakuna maoni :
kipa wa yanga, Juma Kaseja anaendelea kufanya vizuri katika mazoezi ya timu hiyo kiasi cha kocha wake Juma Pondamali kutamka wazi kwamba Deo Munishi ‘Dida’ aliyeko Taifa Stars ana kazi ya kufanya ili apate nafasi kikosi cha kwanza.
Katika mazoezi ya jana Jumatatu ya Yanga, Kaseja alifanya vizuri kwa kuzuia mipira sita iliyoelekezwa langoni kwake na mshambuliaji Genilson Santana Santos ‘Jaja’ na kuwazidi mipira ya kumzidi mipira ya kuokoa mwenzake Ally Mustapha ‘Barthez’.
Pondamali aliliambia Mwanaspoti kuwa, Kaseja ameonyesha uwezo mkubwa tangu kuanza kwa mazoezi chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo ‘The Chosen One’ hali inayoweka wakati mgumu juu ya nani kipa namba moja. “Kaseja nimemuona anafanya vizuri sasa mpaka napata wakati mgumu kuhusu nani atakaa langoni kwani Dida naye anatakiwa afanye kazi ya kunishawishi ili acheze,” alisema Pondamali.
Hadi anakwenda Taifa Stars, Dida ndiye aliyekuwa kipa chaguo la kwanza katika kikosi cha Yanga akifuatiwa na Kaseja halafu Barthez alikuwa chaguo la tatu la kocha aliyeondoka Hans Van Der Pluijm.
Naye kiungo wa zamani wa Yanga, Salvatory Edward ndiye atakayekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo. Tangu kuanza kwa mazoezi ya timu hiyo, Salvatory amekuwa akimsaidia kazi sambamba na Leonardo Neiva wa Brazil.
“Salvatory ndiye msaidizi wa Maximo kwa sasa mpaka hapo uongozi utakaposema vinginevyo,” alisema mmoja wa maafisa wa Yanga.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni