Alhamisi, 24 Julai 2014
MOURINHO AANZA MBWEMBWE
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anatazamia kuitawala Ligi Kuu baada ya kumsajili Cesc Fabregas, Diego Costa na Filipe Luis
.
Mourinho alitumia karibia pauni milioni 80 kuwaleta watatu hao Stamford Bridge kutoka La Liga, ambapo Fabregas alionekana kutohitajika Barcelona huku Filipe Luis na Diego Costa wakiiongoza Atletico Madrid kushinda taji la ligi.
“Timu hii imekuwa timu ya ushindi kwa misimu kumi inabadilika hatua kwa hatua, tumenunua wachezaji wapya na tunajaribu kuijenga kwa miaka kumi ijayo” alisema Mourinho akiwa na timu ya Chelsea mjini Velden, Austria.
“Mwaka uliopita tulifika nusu fainali, na ulikuwa msimu wa mpito”, aliongeza.
“Tulikuwa na timu yenye wachezaji wadogo kwa wakati ule ila, tuliweza kufika nusu fainali na walikuwa wanacheza ili kushinda mashindano”.
“Nafkiri msimu huu tutakuwa na nguvu zaidi, wachezaji wadogo wenye uzoefu, wana nguvu na wako tayari kupambana kwa ajili ya mataji,” alisema.
Pamoja na kusifia ushindani wa Ligi Kuu, Mreno huyo , 51, alisema asingetua Stamford Bridge kama asingekuwa na fikra kuwa Chelsea wataweza kushinda Ligi Kuu msimu ujao.”
Kama nisingefikiria hivyo basi ningerudi nyumbani na kuacha mtu mwingine achukue timu,” alisema kocha huyo wa Chelsea.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni