Nahodha wa England na club ya Liverpool Steven Gerrard hatimaye ametundika daruga kuichezea timu ya taifa lake la England akiwa na miaka 34. Gerrard amejiimarisha kwenye kikosi cha uingereza tangu mwaka 2000 walipoipiga Ukraine kwa mabao mawili kwa nunge.
Kiungo huyo wa Liverpool amesema aliufurahia muda wote alipoichezea timu ya taifa na kwa kweli ni siku ya masikitiko kwake.
Hivi sasa Gerrard atakuwa katika nafasi za juu za ubalozi katika chama cha soka cha England.
Anastaafu akiwa amecheza michuano mikubwa sita na kufunga mabao 21. Na hivyo kushika nafasi ya tatu baada ya Peter Shilton na David Beckham.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni