Ijumaa, 25 Julai 2014
Henry awatoa ushamba Gunners
Mkongwe wa zamani wa washika bunduki wa jiji la London klabu ya Arsenal Thierry Henry alipata fursa ya kujumuika na kikosi chake zamani ambacho kipo jijini New York kwaajili ya kujifua na kujiweka fiti kwa msimu mpya wa ligi ya Uingereza 2014/2015.
Katika ziara hiyo Henry anayecheza klabu ya New York Red Bull kwasasa, alikuwa kama mwenyeji wa jiji katika kuhakikisha vijana wa mzee Wenger haingi katika vyoo vya kike.
Pia baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza akiwemo Jack Wilshire, Aaron Ramsey, Gibbs na Rosicky walipata nafasi ya kucheza basketball pamoja na legend wa klabu yao kama picha zinavyoonesha.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni