Ijumaa, 25 Julai 2014
PEREZ : USAJILI KAMA KAWA, PESA IPO
Rais Los Blancos Florentino Perez amedai kuwa hanampango wa kusitisha kufanya usajili wa mastaa wengine katika kikosi cha Real Madrid msimu huu wa kiangazi.
‘Nitaendelea kujaribu kuongeza mastaa katika kikosi chetu mpaka tarehe ya mwisho ya kufunga dirisha la uhamisho katika majira ya kiangazi
Tayari tumeshafanikiwa kukamilisha usajili wa Toni Kroos pamoja na James Rodriguez lakini lengo letu kama klabu ni kuhakikisha tunaendelea kuleta majembe kwa ajili ya msimu ujao
Kama unahitaji mafaniko ya vikombe katika kila mwisho wa msimu , hunabudi kuachana na tabia za ubahili, mimi naamini kama unahitaji pesa bhasi hunabudi kutoa pesa’.
Hayo ndio maneno aliyozungumza raisi huyo katika mkutano wa waandishi wa habari, ambapo mashabiki wengi wasoka wanasubiri kuona usajili huo jinsi utakavyo fanya kazi, huku mechi ya mahasimu wao Barca maarufu kama El Clasico ikisubiriwa kwahamu .
Ambapo safu ya maangamizi ya Real ikiundwa na Ronaldo, Kroos, Rodriguez, bale, na Benzema huku ile ya Barca ikiundwa na Messi , Suarez, Neymar, Iniesta, na Pedro kwahiyo unaambiwa lazima siku ya mechi hiyo nyasi zitawaka moto.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni