Sports and Entertainment

Ijumaa, 25 Julai 2014

Wakulima Tanga na Morogoro wapata soko Thailand

Hakuna maoni :
Wakulima wa mikoa ya Tanga na Morogoro nchini wamepata soko la uhakika la zao la mahindi kufuatia shirika moja la CPP linalosimamiwa na serikali ya Thailand kuingia mkataba na wakulima hao wa kuzalisha mahindi ya njano kufuatia shirika hilo kuhitaji tani zaidi ya milioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya kwenda kusindika na kutengeneza vyakula vya mifugo katika nchi za asia.
 
Wakizungumza katika uzinduzi wa mkataba huo ambao katika nchi za afrika ndio wa kwanza kuzinduliwa nchini baada ya ofisi ya rais na ile ya waziri mkuu kuridhia mkataba huo ili kuwapunguzia adha wakulima kukosa soko la mazao ya chakula sanjari na kujitosheleza kwa chakula, viongozi wa wizara husika wamesema kwa kuanzia watapatiwa mbegu, wataalam pamoja na pembejeo za kilimo ili waweze kuzalisha mahindi hayo kwa ufanisi chini ya usimamizi wa wizara ya kilimo, chakula na ushirika.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Muheza Bi.Subira Mgalu akisoma taarifa ya mkuu wa mkoa wa Tanga kwa niaba yake amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Kikwete alipofanya ziara hivi karibuni mkoa wa Tanga na kuwataka wakulima kujiunga na vyama vya ushirika ili waweze kulima kwa tija na suala la masoko limepatiwa ufumbuzi ili iwe fursa kwao kuondokana na umasikini.
 
Akielezea fursa hiyo Rais wa shirika la CPP Bwana Winay Heiman amesema wameonelea kuwa waanze mradi huo wa mahindi ya njano katika nchi za afrika hususani kwa Tanzania kabla ya kuwashirikisha nchi jirani ya Kenya kufuatia balozi wao kuomba huduma hiyo iweze kuwafikia wakenya kwa sababu ya uhaba mkubwa wa chakula unaowakabili wananchi wake.
 
                      

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni