Ijumaa, 25 Julai 2014
JAJA : Simba Hawaninyimi Usingizi, Owino ampa makavu
STRAIKA wa Yanga Mbrazili, Genilson Santos ‘Jaja’ sasa anaijua vizuri Simba baada ya kusikia maneno mengi kuhusu timu hiyo ambapo ametamka kuwa mechi dhidi yao itampa heshima Tanzania nzima. Lakini beki wa Msimbazi, Joseph Owino amesikia maneno yake akacheka halafu akamjibu.
Jaja alisema kuwa: “Unapocheza kwenye timu kubwa ambayo ina wapinzani wake kama Yanga na Simba na kufanikiwa utaheshimika sana, kitu kikubwa unapokuwa kwenye ligi unatakiwa kutambua kuwa timu zote ni mpinzani wako mkubwa zaidi mechi dhidi yake unatakiwa uchukulie kwa ukubwa.”
“Mimi binafsi nitalenga kuipa ushindi Yanga mbele ya wapinzani kama Simba na pia nitajituma kwenye mechi zote,” alisema. Straika huyo pia alisema kuwa anaufananisha upinzani kati ya Simba na Yanga na ule wa kule Brazil kama vile Fluminence dhidi ya Flamingo, Corinthians na Sao Paulo na Flamingo dhidi ya Vasco da Gama.
“Upinzani wa Simba na Yanga nina uhakika unavuta wengi, lakini tumuombe Mungu mambo yaende vizuri ili siku ifike na tucheze,” alisema na kuwataja beki Juma Abdul, kiungo Nizar Khalfan na Andrey Coutinho kuwa wanamfurahisha sana.
“Abdul anapiga krosi nzuri ambazo zina mazingira ya kufunga na aina ya krosi anazopiga huwa zinawapa wakati mgumu mabeki, Nizar ni profeshno kwa kweli, anajua kupiga pasi na kukutengenezea nafasi wakati mwenzangu Coutinho naye ni mzuri. Kiukweli wachezaji wote wananipa wakati mzuri kuzoea na kucheza soka Tanzania.”
Beki tegemeo wa Simba Owino amesikia maneno ya Jaja na anajua kwamba anapewa mazoezi ya kufunga kwa vichwa, sikia alivyomjibu; “Mimi na hata mwenzangu Donald Mosoti hatutishwi na mazoezi anayopewa Jaja ya kupiga vichwa. Mimi binafsi ni mpigaji mzuri wa mpira kwa vichwa na kwa hilo hatuna shaka naye, anayeweza kuwa na madhara makubwa ni Cannavaro (Nadir Haroub). Yanga hakuna ambaye anajua kufunga kwa vichwa kama Cannavaro, wengi wao ni wa mipira ya chini.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni