Alhamisi, 24 Julai 2014
michuano ya jumuiya ya madola yaanza Scotland
Mashindano ya Jumuiya ya Madola yameanza leo mjini Glasgow Scotland na kufunguliwa rasmi na Malkia Elizabeth wa Uingereza ambaye pia ni mkuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya madola
Zaidi ya wanariadha elfu tatu wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo yatakayodumu kwa muda wa majuma matatu yajayo
Australia ndio nchi ambayo imetuma kikosi kubwa zaidi katika mashindano haya ya mwaka huu
Takwimu rasmi zinasema kuwa Australia inawakilishwa na zaidi ya wanariadha 400
Mataifa yote nchi wanachama wa muungano huo kutoka kanda ya Afrika Mashariki na Kati yamewakilishwa kwenye mashindano ya mwaka huu
Ushindani mkali unatarajiwa katika fani mbali mbali za michezo na macho yote ya Dunia yatakuwa katika shindano la riadha ambalo litatumiwa na mataifa mengi kuchagua vikosi vyao vitakavyoshiriki katika mashindano ya mabara na hatimaye Kombe la Dunia
Mashindano haya yataanza rasmi hiyo kesho huku wanariadha kadhaa wa Afrika Mashariki wakijibwaga uwanjani kuchuana na wapinzani wao katika raundi ya kwanza ya mashindano ya Judo, Masumbwi na Table tennis
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika Mashariki ili hii laana ya kichwa cha uwenda wazimu katika michezo tuivunje
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni