Jumamosi, 19 Julai 2014
LEBRON JAMES AWATOA MACHOZI MASHABIKI,,,,AHAMA MIAMI HEAT
Uhamisho wa mcheza kikapu aliyekuwa akiichezea timu ya Miami Heat, Lebron james, umeonekana kuzua gumzo baada ya mchezaji nyota huyo kuamua kurejea katika timu yake ya zamani ya Cleveland Cavaliers kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuitumikia Miami katika misimu minne na kuiwezesha kutwaa ubingwa wa NBA mara mbili pamoja na kupata Tuzo ya MVP mara nne mfululizo.
Maamuzi ya Lebron yameoneka kutowapendeza baadhi ya mashabiki na wachezaji wa Miami akiwemo Dwayne Wade ambaye ameonyesha kusikitishwa na uamuzi uliofanywa na swahiba wake wakati kwa upande wa Chris Bosh amenukuliwa akisema anadhani bado wanauwezo wa kuwa wapinzani bila ya uwepo wa Lebron.
”Kama Rafiki na mchezaji mwenzangu, Nasikitika kuona ndugu yangu Lebron anaondoka na kuanza safari mpya,alisema Wade. Mwaka 2010, tuliamua kuhamia Miami kwa lengo moja la kutwaa ubingwa na tulifanikiwa. Tulikuwa marafiki tangu mwanzoni tulipojiunga na tuliweka malengo madhubuti katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Ushirikiano wetu daima utakuwa wa kipekee”.
Mashabiki na wapenzi wa Lebron James wategemee kumuona nyota wao huyo akiwa kwenye jezi mpya yenye namba 23 mgongo ambayo ilikuwa jezi yake ya awali kabla ya kuhamia Heat mwaka 2010 na kupewa jezi namba 8.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni