Sports and Entertainment

Jumamosi, 19 Julai 2014

yule mfungwa kipenzi cha akina dada akutwa ameuawa

Hakuna maoni :


Jeremy MeekMfungwa handsome boy aliyekuwa kivutio kikubwa cha wakina dada wengi kufuatia picha yake(mugshot) kuzagaa mitandaoni, mwili wake umekutwa na mapolisi wa Stockton eneo la Dayton magharibi mwa mji wa Stockton ukiwa na majeraha kadhaa yaliyomsababishia apoteze maisha muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.
Uchunguzi wa polisi umesema kwamba Meek aliachiwa huru usiku wa Jumanne(Julai 14) na kwenda nyumbani kwa mama yake ambapo usiku wa kuamkia Jumatano mwili wake ulikutwa umelala chini ya barabara ukiwa umejeruhiwa na kitu kinachodhaniwa ni risasi au kisu kwa kile kilichotajwa kuwa ni ugomvi uliotokea baina yake na mkewe aitwaye Lashada.
Polisi imefanikiwa kumkamata Lashanda Meek pamoja na  ushahidi wa bastola  na gari dogo alilotumia kukimbia nalo eneo la tukio kwenye nyumba aliyokuwa amejificha.
Mkuu wa polisi wa Stockton, Tom Morris, amesema kwa sasa Lashada anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya mkoa na baada ya hapo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni