Jumamosi, 26 Julai 2014
sudan kusini yakabiliwa na njaa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini kama mbaya zaidi kuwahi kuonekana duniani na kuyataka mataifa ambayo yaliahidi kutoa msaada wa zaidi ya dola millioni 600 kutoa fedha hizo.
Pia shirika hilo limeonya kuwa vita vinavyoendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi huenda vikasababisha baa la njaa nchini humo.
Shirika la chakula duniani WFP limesema kuwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa watoto 50,000 huenda wakapoteza maisha yao kutokana na utapia mlo mwaka huu huku theluthi moja ya raia wakikabiliwa na na viwango hatari vya njaa.
Chanzo: BBC Swahili.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni