Sports and Entertainment

Ijumaa, 1 Agosti 2014

2FACE IDIBIA AITIKISA BILLBOARD CHART

Hakuna maoni :
Muziki wa Nigeria umeendelea kupasua anga za kimataifa kufuatia albamu mpya ya staa wa African Queen, 2Face Idibia inayoitwa ” The Ascension” kutajwa na jarida la Billboard kama albamu iliyofanya vizuri sokoni katika wiki ya kwanza ikikamata nafasi ya 12.


The Ascension ambayo ni albamu ya sita kwa 2face iliyotoka Julai 21 mwaka huu chini ya lebo ya 960 Music Group, imeweza kuweka rekodi ya kuwa albamu ya kwanza kutoka Nigeria kukamata nafasi za juu kwenye chati za Billboard zilizotolewa hapo jana(Julai 31).
2face amewashukuru  mashabiki na wale wote waliomsapoti kwa namna moja au nyingine sambamba na kupata pongezi za nguvu  kutoka kwa mama watoto wake, Annie Macaulay-Idibia kupitia ukurasa wake Instagram
”I Am Screaming thank YOU JESUS!!!! This is the 1st time EvER In the world, any Nigerian artist achieved this!!! Record-Breaking! 2face Idibia’s ‘The Ascension’ Album Is Currently The 12th Top Selling Album In The World – Music ” aliandika Annie
Vigezo muhimu vinavyozingatiwa na Billboard katika kupata albamu zinazouza zaidi ni pamoja na kutazama mauzo ya albamu husika, watu wanaoipakua mtandaoni, muda wa hewani kwenye redio, ziara(Touring) na muingiliano wake kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Vevo, Youtube, Spotify na mengineyo.
2Face-Idibia-billboard-chart
 Chati ya  Billboard ikionyesha albamu zinazokimbiza kwa mauzo sokoni huku ya 2face ikiwa kwenye nafasi ya 12 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni