Jumatatu, 4 Agosti 2014
TETESI ZA USAJILI MAJUU
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema hana mpango wa kumchukua Mario Balotelli kutoka AC Milan, baada ya mchezaji huyo kuhusishwa na Anfield (Daily Mirror)
, Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa Porto Eliaquim Mangala, 23, kwa pauni milioni 32 (Manchester Evening News),
Tottenham wapo karibu kufikia makubaliano na Villareal kumsajili beki wa kati Mateo Musacchio, 23, (Times)
, meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kuwapa Southampton winga Southampton winga Nacer Chadli ili kuwashawishi kumchukua Morgan Schneiderlin (Sun)
, meneja wa West Ham Sam Allardyce anataka kumchukua winga wa Manchester United, Wilfried Zaha, 21 (Sun),
West ham pia wanamtaka Peter Crouch, 33, kutoka Stoke City kuziba pengo la Andy Carroll ambaye ni majeruhi (Daily Express),
meneja wa Southampton, Ronald Koeman anataka kumsajili winga chipukizi wa Manchester United Demetri Mitchell kwa mkopo (Daily Mirror),
AC Milan wanamtaka kipa wa Liverpool Pepe Reina, lakini kipa huyo anataka mshahara mkubwa (Daily Mail),
meneja wa Crystal Palace, Tony Pulis anamyatia beki wa Stoke Marc Wilson (Daiky Star), Newcastle wana matumaini ya kumsajili beki wa kati kutoka Nottingham Forest Jamaal Lascelles, 20, kwa pauni milioni 3 (Daily Mirror),
Tottenham wanafikiria kumchukua Samuel Eto'o, 33, baada ya kuondoka Chelsea (Tuttosport),
Liverpool wanakaribia kumsajili Alberto Moreno, 22 kutoka Sevilla kwa pauni milioni 16 (AS)
, kiungo Marco Reus, 25 ambaye amehusishwa na kwenda Bayern Munich na Liverpool atabakia Borussia Dortmund kwa msimu mwingine (L'Equipe)
, mkataba wa pauni milioni 60 kati ya Real Madrid na Paris St-Germain juu ya winga kutoka Argentina Angel Di Maria huenda ukakamilika katika siku mbili zijazo (Marca)
, Liverpool imetoa dau la pauni milioni 5 kutaka kumsajili beki wa Barcelona Dani Alves, 31 (Mundodeportivo), Wolfsburg wanamtazama mshambuliaji wa Chelsea Fernando Torres, 30, baada ya kushindwa kumchukua Romelu Lukaku, 21 aliyekwenda Everton (Bild),
Real Madrid wanataka kumchukua kiungo wa Wolfsburg Luiz Gustavo, 27 iwapo Sami Khedira ataondoka. Arsenal na Chelsea wanamfuatilia kiungo huyo (Bild)
, beki wa kati kutoka Brazil, Miranda amekataa kwenda Cheslea, Manchester United na Barcelona, na badala yake atasalia Atlètico Madrid (Marca),
Juventus wanaonekana kukata tamaa ya kumzuia Arturo Vidal baada ya Manchester United kutoa pauni milioni 40. Mabingwa hao wa Italia watamtaka Nani na Javier Hernandez katika mkataba huo (Corriere dello Sport).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni